Karibu Bonasi

Katika ulimwengu huu ulioendelea, tasnia ya kubashiri michezo mtandaoni imekuwa yenye ushindani hadi kiwango ambacho waendeshaji wa tovuti wanajitahidi kupata wateja wapya. Kufikia sasa Karibu Bonasi imefanya maajabu makubwa kwani wachezaji wanapenda kutumia fursa ya pesa za bure wanazopewa na waendeshaji wa tovuti.

Nini Maana ya Karibu Bonasi?

Kama inavyojulikana, karibu bonasi ni ofa ya kwanza inayotolewa na waendeshaji wa tovuti mtandaoni ili kuvutia wateja kujiunga na tovuti yao. Mchezaji anayo haki ya kudai karibu bonasi mara tu taratibu za kujisajili kukamilika. Kumbuka kwamba karibu bonasi hutolewa mara moja tu bila upendeleo wowote. 


Aina za Karibu Bonasi

Wachezaji wapya wanakumbushwa kwamba karibu bonasi inaweza kutolewa katika mifumo tofauti lakini zote hukupa wewe mchezaji fursa zaidi ya kutengeneza beti za ziada na kushinda zaidi.
 • Aina ya karibu bonasi inayotumiwa mara nyingi ni amana bonasi. Ofa hii hutolewa kwa kukuongezea asilimia ya amana ya awali ya mchezaji.  Amana bonasi kawaida huanzia 25% hadi 100% na wakati mwingine 200% kwa baadhi ya waendeshaji. Mfano ikiwa umeweka amana ya Tsh 100,000, mwendeshaji atakuongezea Tsh 100,000 kama ofa ya 100%. Walakini, karibu bonasi kawaida huwa na kikomo hadi kiasi fulani kwa hivyo ni bora kupiga jicho kwenye vigezo na masharti.

 • Bonasi ya beti za bure hufanyika kwa njia sawa kama amana bonasi katika viwango vya thamani lakini beti za bure hazitolewi moja kwa moja baada ya amana ya kwanza. Waendeshaji  wengi wa tovuti mtandaoni hutoa beti za bure baada ya wateja wapya kuweka amana yao ya kwanza na kuweka beti yao ya kwanza kwa thamani fulani ya odds aliyopewa. Vigezo na masharti ya beti za bure yanaweza kutofautiana kutoka kwa waendeshaji tofauti kwa hivyo hakikisha unasoma na kuelewa masharti yaliyowekwa kwenye ofa.

 • Bonasi ya kurudishiwa hisa ni moja ya aina inayothaminiwa na wachezaji wengi wa michezo wa kubashiri mtandaoni. Kanuni yake ni rahisi kueleweka, baada ya kusajili na mwendeshaji wa tovuti ya kubashiri na beti yako ya kwanza ambayo uliiweka ikapoteza, mwendeshaji wa tovuti atakupa ofa ya kukurudishia hisa yako yote kwa ujumla au wakati mwingine sehemu ya hisa.

 • Baadhi ya waendeshaji wanaweza kutoa odds zilizoboreshwa kwa baadhi ya matukio na wachezaji wanaweza kutumia fursa hii kutengeneza beti nzuri na kujiongezea nafasi za kushinda kwa kutumia ofa hio ya odds. 


Vitu Vya Kuzingatia Unapochagua Karibu Bonasi

Aina za karibu bonasi hapo juu ni njia nzuri ya kuongeza salio la mchezaji lakini daima ni wazo zuri kuelewa kikamilifu dhamana utakayolipa kabla ya kukubali ofa hio. Kuelewa vigezo na masharti itakusaidia kupata ofa bora zaidi kwenye soko. 
 • Unaweza kugundua kwamba kwa baadhi ya waendeshaji ili kupata karibu bonasi unatakiwa kwanza uweke amana yenye kiwango cha chini kilichowekwa na mwendeshaji. Kiwango cha chini cha amana kinaweza kutofautiana kutokana na tovuti na tovuti. 

 • Hii inaweza kuwachanganya wachezaji wengi lakini wazo la msingi ni rahisi, kiwango cha chini cha kufuzu beti ni tofauti na kiwango cha chini cha amana. Hapa beti inayostahiki kiwango cha chini inamaanisha kiwango cha chini cha hisa unayostahili kuweka ili ustahiki kupata beti ya bure au aina nyingine yoyote ya ofa. 

 • Masharti ya kubashiri ndio sehemu ngumu zaidi ya vigezo na masharti ya karibu bonasi. Mwendeshaji wa tovuti anaweza kuweka vigezo na masharti juu ya ni mara ngapi unahitaji kuweka beti kabla hujaweza kutoa salio lolote lililotokana na bonasi.

 • Ni wazi kuwa karibu bonasi yako haitadumu milele na kwa hivyo kila aina ya karibu bonasi ina kipindi cha kumalizika. Waendeshaji wa tovuti kawaida huweka muda mdogo ambapo unaweza kupata ofa yako baada ya kuunda akaunti. Ni vizuri kutumia karibu bonasi yako wakati bado ipo.

 • Unaweza kukutana na vigezo kwa baadhi ya waendeshaji kwamba karibu bonasi inatumika kwenye baadhi ya masoko peke yake au kwenye matukio fulani tu.


Jinsi ya Kupata Bonasi Yako ya Kubashiri Michezo ya Karibu Bonasi

 • Kufanya utafiti inaweza kuwa si jambo la muhimu kwako lakini ni bora kujua ni nini kila mwendeshaji anatoa kwa wateja wake. Tumia muda wako kutembelea tovuti tofauti za kubashiri na kulinganisha bonasi ya kila mwendeshaji itakayokufaa. Vitu vingine vya kuzingatia vinaweza kujumuisha idadi ya masoko, matukio, odds na unaweza pia kuzingatia kuangalia kupatikanaji wa tovuti kupitia simu ya mkononi.

 • Daima ni bora kuelewa vizuri ni kitu gani unaenda kujiunga nacho. Vigezo na masharti yoyote ya tovuti ni sehemu ya lazima kusoma. Soma kwa uangalifu mahitaji ya kubashiri, kiwango cha chini cha amana za kwanza, kikomo cha kutoa pesa nk.

 • Baada ya kufanya utafiti wako na kuelewa kikamilifu vigezo na masharti ya tovuti uliyoichagua, utahitaji kutengeneza akaunti ili kuweza kupata karibu bonasi yako. Mchakato wa kijiunga itakuchukua dakika chache na kwa baadhi ya tovuti, utahitaji kukubali kupokea ofa ya karibu bonasi. 

 • Baada ya kuwa na akaunti na tovuti ya kubashiri, sasa unaweza kuweka amana yako na kudai karibu bonasi yako kutoka kwenye tovuti labda kama hujakubali kupokea ofa hio.

 • Tumia amana yako na salio la bonasi vizur na utengeneze beti za ushindi, Kila la Kheri!!